Monday, March 14, 2011

KWA BABU HUDUMA KAMA KAWA HABARI ZAIDI KUPITIA ITV & STAR TV

                                          Video toka ITV-Loliondo

                                        Video toka Star Tv--Loliondo

Sunday, March 13, 2011

Jumapili njema..

 >

Friday, March 11, 2011

JAPAN YAKUMBWA NA TSUNAMI

Japan imekumbwa na tetemeko kubwa la bahari maarufu kama Tsunami ambalo limesababisha uharibifu mkubwa wa mali na maisha ya binadamu mapema leo.Tetemeko hilo  kubwa kiasi cha 8.9 magnitude limeripotiwa kuathiri sehemu kubwa ya maeneo ya pwani kaskazini mashariki mwa Japan ambako mamia ya watu wana hofiwa kufa kwa kuangukiwa na nyumba na mafuriko makubwa ya maji yaliyo tapakaa toka baharini na kubomoa nyumba,kuzamisha magari,meli na kusababisha moto mkubwa baadhi ya maeneo.

Tetemeko hilo  la kihistoria limepelekea kuzimwa kwa mitambo minne ya Nuclear ambayo hutumika kufua umeme wa Gigawatts 11.Halihiyo imepelekea maeneo mengi kuwa bila umeme.Japan  ni moja kati ya nchi zinazo zalisha umeme kutumia Nuclear na asilimia 30 ya umeme wake hutokana na nishati hio.


                            (Ramani ya Japan)


Wataalam wa mitambo hio wame tahadharisha kuhamisha watu wote karibu na mitambo hio iliopo pwani ya Japan maeneo ya Fukushima na Fukui kwani tetemeko limeathiri mitambo hio na kuweza kupelekea uwepo wa mionzi inayo athiri watu au hata kusababisha vifo.Kudhibiti hilo marekani imeripotiwa kupeleka kipozeo cha mitambo hio baada ya kilichokuwepo kuharibiwa kutokana na tetemeko hilo.

Kwa picha zaidi na Video toka BBC  bonyeza kwenye link :http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-pacific-12709847. Pia videoa toka RT angalia chini

                                                                 RT (2 mins Video footage  11/03/2011)

Wednesday, March 9, 2011

50 INCH PANASONIC PLASMA TV OFFER


Brand new Original Panasonic plasma Tv 50 Inch (127cm) for sale ***Made in the United Kingdom (UK)*** Very cheap!!!!For Serious inquiry please email: rijaki@ymail.com OR Call: 0653624150;Location: Dar es salaam.Delivery:Free (In Dar es salaam only
 

Product Features and Technical Details
Product Features

• VIERA HD Ready 50-inch Plasma TV
• 100Hz Double Scan for ultra-smooth picture quality
• Dynamic Contrast 2,000,000:1
• VSmart Networking with VIERA Link and VIERA Image Viewer (integrating Photo and Video)
• Game Mode, V-Audio Surround

TV Tuner:
Integrated Tuners: PAL-I, DVB-T
Tele text Reception: 1000P Level 2.5, FASTEXT/LIST

Display
Screen Size: 50" (127 cm) diagonal
Panel: G13 Progressive HD Plasma Display Panel with Tough Panel
Viewing Angle: Viewing Angle Free
Resolution: 1,024 x 768 (16:9)
Applicable Scanning Format:
FULL-HD 1125: (1080)/50i, 1125 (1080)/60i, 1125 (1080)/24p (HDMI only), 1125 (1080)/50p (HDMI only), 1125 (1080)/60p (HDMI only)
HD: 750 (720)/50p, 750 (720)/60p
SD: 525 (480)/60i, 525 (480)/60p, 625 (576)/50i, 625 (576)/50p
Contrast Ratio (in dark surroundings): 2,000,000:1 Dynamic
Moving Picture Resolution: 720 lines
Intelligent Frame Creation: 100 Hz Double Scan
24p Smooth Film/Plaback Plus/Playback: 24p Playback
Shades of Gradation: 4,096 equivalent steps of gradation
Deep Colour (10/12-bit): yes
3D Colour Management: yes
Picture Mode: Dynamic/Normal/Cinema/True Cinema/Game/Photo
Vreal: Vreal 5

Sound
Speakers: 2 x 10 watt 2 Speakers
Sound Mode: Music/Speech/User
Virtual Surround: V-Audio Surround
Dolby Digital Out/CoNEQ: Dolby Digital

Input/Output
CI (Common Interface)*: yes
VIERA Image Viewer: yes (AVCHD/SD-VIDEO/JPEG playback)
HDMI Input/ Support Feature: 3 (1 side, 2 rear)/ Audio Return Channel (Input 2)
Composite Video Input: AV3: RCA phono type x 1 (side)
Audio Input (for Video): AV3: RCA phono type connectors (L, R) (1 set, side)
Component Video Input: RCA phono type x 3 [Y , PB, PR] (rear)
Audio Input (for HDMI, PC, Component) RCA phono type connectors (L, R) (1 set, rear)
21-Pin Input/output: AV1: AV In/Out, RGB In, Q-Link (rear) / AV2: AV In/Out, S-Video In, RGB In, Q-Link (rear)
Analogue Audio Out: RCA phono type connectors (L, R) (1 set rear)
Digital Audio Output (Optical): yes
Headphone Jack: 1 (side)
Features
EPG: yes
VIERA Tools: yes
VIERA Link: yes (HDAVI Control 5)
Multi Window: PAT
C.A.T.S. (Contrast Automatic Tracking System): yes
Game Mode: yes
Q-Link: yes
Off Timer: yes
Child Lock: yes

General
Wall mountable: yes
Power Save Mode: yes
Power Supply: AC 220 - 240 V, 50/60Hz
Rated Power Consumption: 265 W
On mode Average Power Consumption: 201 W
Standby Power Consumption: 0.4 W
Dimensions (W x H x D) (w/o stand): 1,218 x 769 x 93 mm
Dimensions (W x H x D) (with stand): 1,218 x 814 x 401 mm
Weight (w/o stand): 31.5 kg
Weight (with stand): 33.5 kg
Boxed product : 40kg
Wall Bracket: TY-WK4P1RW (not included)
Remote Control:Yes (included)

YALIYO JIRI-LOLIONDO



                                                ITV  na Taarifa kuhusu kinacho endelea Loliondo



Hali livyo hivi sasa Loliondo kwa babu.

Hakika huyu babu anahitaji msaada wa haraka maana pamoja na watu kwenda wakitembea wenyewe, kuna wale wagonjwa walio bebwa ambao bila shaka hali zao sio nzuri.Si hivyo tu pia hali ya usalama kufuatia kugombea huduma kunaweza zua jambo lingine la hatari.Kila mtu anataka kuishi, kila mwenye mgonjwa angependa mgonjwa wake atibiwe mapema iwezekanavyo ila kwa uwingi huu wawatu hakika huyu babu hataweza kumudu akiwa hana msaada  wa ziada kwani watu hawataweza vumilia kulala nje kila siku.Si hivyo tu kuna wagonjwa ambao kwa msongamano huo wa watu lazima watapoteza maisha.Serikali ichukulie jambo hilo uzito wa ziada ikiwa ni pamoja na kuhakiki ukweli wa tiba hio. Ni hayo tu kwa leo.

Monday, March 7, 2011

BABU ANAYE SADIKIKA KUTIBU UKIMWI AFURISHA WATU-ARUSHA

Babu mmoja kwa jina Ambilikile Mwasapile (76) wa Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha amejipatia umaarufu wa ghafla baada ya kugundulika anatibu magonjwa lukuki ukiwemo UKIMWI.Babu huyo ambae inasaidikika ni mchungaji mstaafu wa kanisa la KKKT-Loliondo amesema mwanzo ilikua ni ndoto ambayo amekua akiiota toka mwaka 1991 ambayo Mungu amemuagiza aponye watu.Ndoto hio imejirudia rudia mpaka Augusti mwaka 2010 ambapo aliamua  kuanza kutoa tiba rasmi kwa gharama ya sh.500 tu.

 

Mpaka sasa maelefu ya watu mbalimbali,vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake wamekuwa wakienda kwa mzee huyo kupata tiba na baadhi wamekili ni TIBA HALISI.Mpaka sasa ni kama kitenda wili machoni pa watu kila mtu akiuliza ni kweli au sio kweli.Kwenye mitandao mbalilimbali kama facebook,blogs,webisites na chatrooms  gumzo ndo hilo japo bado hawaamini kama ni kweli na wanasema kama ni kweli na wao wataenda

 

Kwa walio ona foleni ni kubwa kupita maelezo katika kufata tiba hio ya asili na huenda babu huyo akavunja rekodi ya utojai tiba asili nchini Tanzania tena kwa muda mfupi. Kama utavyo ona picha hapo chini watu ni wengi sana kama nilivyozitoa Facebook.

 

Siku zote mimi huwa nasema kwa watu wa karibu UKITAKA KUJUA KAMA KUNA WATU WANAUMWA NENDA HOSPITALI NA UKITAKA JUA KAMA WATU WANAKUFA NENDA MAKABURINI.Bila hivyo hutajua labda kama anaye umwa ama kufa ni ndugu ama jirani au wale ambao utaona ama kusikia kupitia vyombo vya habari.

 

        Msafara kwenda kwa babu


    Babu akiwa amezungukwa na watu waliofata tiba pamoja na kushangaa

           msafara ndio kama hivi ( babu asababisha foleni)

Sunday, March 6, 2011

LIVE TOKA ENEO LA TUKIO..

Katika kupita pita kupata habari hapa na pale nikaja kutana na habari ya mada kuhusu  urembo wa wasichana wakitanzania dhidi ya wale wanaijeria kupitia http://u-turn.co.tz/index.php?start=10. post ya tarehe 01/03/2011. Mada hio iliambatana na pichaa kadhaa za wasichana wa kitanzania yamezaa maoni lukuki yaliyo katika mtindo wa kubishana/kujibishana tena kwa maneno makali. Mpaka sasa haijajulikana nani ameanzisha malumbano hayo makali  pamoja na kutuma picha kwa blogger aitwae Linda wa Nigeria.

Wengi wanasema pengine imekua gumzo kwa mshindi wa BBA (Kevin-Nigeria) kumuoa Mtanzania (Elizabeth) wakiuliza kwani Nigeria wasichana wazuri hakuna? kwenye comments za wanaijeria wakaka wanasema wadada wakitanzania hujipendekeza kwao kwa uzembe wakutaka vya bure na wao ndio wanawachukua ila si kwamba ndio wazuri.Mimi sijui ukweli ndio upi zaidi ya kusikia wasichana (Baadhi) wakitanzania kuwasifia wanaijeria ndio wanaume wa ukweli na wanajua kujali (mimi sina maoni juu ya hilo)

Ukisoma maoni yaliyo tolewa wameitukana hadi Tanzania kama nchi (Too bad) hasa katika swala zima la umasikini na kwamba wengi wetu ni vihiyo,washamba,lugha haipandi na masikini wakubwa.Hata hivyo wa kaka wa kinaijeria wamesema kuwa wasichana wao ni wazuri kupita wakitanzania ila kwakua hawa wa Tanzania ni cheap ndio huwachukua.Wakati huo huo wasichana wakinaija wamesema (kupitia maoni) kua huyo aliye olewa na mume wao (yaani kaka wa kinaija) basi watakula naye sahani moja!

Malumbano hayo ambayo hayana miguu wala kichwa yamezaa maoni mengi  kupita kawaida katika blog hio kwa kulaani hio mada ya kulinganisha kazi ya Mungu (ambayo siku zote haina makosa) na kupelekea kila mmoja kwa nafasi yake kujitetea  tena kwa hasira na Lugha kali.

Blog  hii inalaani yeyote aliyepelekea kuazishwa kwa mjadala huo duni na kutoa wito wa kutoa mada za kujadili mambo ya msingi na maendeleo na sio 'Urembo/beauty' ambao uko subjective kwa kiasi kikubwa kwani kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo tofauti katika Urembo wahenga walisema 'Beauty is according to the eyes of the beholder'. Kwahio tujadili mambo mengine sio haya yanayo lete mabishano yasiyo na umuhimu.

 Sitaki kuongea mengi ili kuona mjadala ulivyokua na maoni ambayo mpaka naandika hapa yamefika 134 ingia hapa: http://lindaikeji.blogspot.com/2011/02/are-tanzanian-women-more-beautiful-than.html

Pia ukitaka ona post na comments za u-uturn  kuhusiana na mada hio hio na comments za watanzania ingia hapa: http://www.u-turn.co.tz/index.php/kwanza/1588-ohoooo-wanaigeria-wanatutafuta#JOSC_TOP