Monday, May 23, 2011

LIMO YA OBAMA MAARUFU KAMA ''BEAST'' YABUMA ZIARANI IRELAND

Gari moja wapo katika msafara wa Obama  huko Ireland yabuma baada ya kugonga tuta nje ya ubalozi wa Marekani jijini Dublin-Ireland.Gari hilo aina ya Cadillac la Mr Obama lenye jina maarufu kama ''The Beast'' Yaani 'Mnyama' kwa kimakonde lilisekana kubeba wataalamu wa ulinzi katika msafara huo wakati Rais wa Marekani Barack Obama akiwa ziarani nchini humo jana tarehe 23/05/2011.

Umati mkubwa wa watu umeshuhudia tukio hilo 'live' ambapo mlio mkubwa ulitokea baada ya chesis lake kugusa tuta na kushindwa kwenda mbele na muda si mrefu waliletewa gari lingine kuendelea na msafara.


Kama uonavyo kwenye video hapo juu hicho ndicho kilichotokea.Limo/The Beast hilo lina  urefu wa futi 18 na uzito wa tani 8 na upana wa chuma cha bodi wa inch 8 halipitishi bomu wala risasi na lina lina oxygen yake ndani.Rais Obama akiwa ndani ya hilo gari nick name yake inakua Cadillac one na sio The Beast.  The beast inasemekana kua na camera kila kona,shotguns na vingine vingi kwa ulinzi zaidi                               


Mafundi wakinasua The Beast iliponasa



The Beast katika mchoro

(chanzo:dailymail)





                                                                                                                                                                            

UNAIKUMBUKA HII??

Hiki kiatu kilikua maarufu sana zamani siku hizi sikioni tena sijui bado kinavaliwa? Na kama kinavaliwa sijui utaanguka mara ngapi kwenye hizi barabara zetu? Hiki huvaliwa na suruali yake (hasa draft) ambayo ni pana kwa chini nyembamba karibia kubana fulani kwenye magoti.Si kila mtu alikua na kiatu kama hiki jina kama sikosei ni Laison (kama kuna jina lingine usisite nitafurahi kulijua). Pia sikumbuki ni miaka gani ila zamani niliweza ona watu wachache wanavaa na ilikua fashion by then.Wewe je umewahi kuona hiki kiatu? je kina kukumbusha nini??

Friday, May 20, 2011

ATI UMASIKINI WA TANZANIA NI LAANA???

Hebu sikiliza mjadala huo hapo chini na useme mtazamo wako kama ni laana au tunajitakia kua masikini? je  kila mmoja wetu katika jamii tunayo ishi anawajibika kwa nafasi yake au ndio tunanyoosheana vidole kuonyesha  kijibanzi kwenye jicho la jirani wakati sisi tuna boriti machoni mwetu? Penye wengi hapa haribiki neno, maswali ni mengi ila kwa sasa tuangalie haya kwanza kama ni laana,tunajitakia,hatuwajibiki,hatuja wezeshwa,uzembe,bora liende,aliye shiba hamjui mwenye njaa au ndio niseme kama wanavyosema kwetu kule ''TUNGAYA SIDA'' YAANI HATUNA SHIDA KABISAA YAANI YOTE SAWA TU?? SEMA USIKIKE!!!

SEHEMU YA KWANZA


SEHEMU YA PILI


CHANZO:MWANAKIJIJI




Thursday, May 19, 2011

DOLLAR MILLION 6 ZAMUOKOA

Hatimaye aliyekua Mkurugenzi wa IMF  Dominique Strauss-khan akubaliwa kutoka rumande kwa dhamana ya Dollar Million 6 ( $6m) na masharti makali ikiwemo kua chini ya ulinzi kutoka kampuni binafsi kwa gharama ya Dollar laki mbili kwa mwezi ambazo ni juu yake,kuwekwa chombo cha kisasa mguuni kitakacho onyesha alipo kwa saa 24 kila siku,kufungwa kwa video camera katika nyumba atakayo kaa na alarms kumzuia asitoke.

Mheshimiwa huyo ambaye mpaka sasa amejihudhuru wadhifa wake kama Mkurugenzi wa IMF kwa takribani miaka minne kutokana na kashfa ya kutaka kubaka mhudumu wa hotel huko Marekani,ataachiwa na kwenda kuishi kwa muda katika nyumba ya muda ambako mkewe Heiress, Anne Sinclair, mwanahabari na  Millionea wa kifaransa amempangishia wakati akisubiri kesi yake kusikilizwa hivi karibuni.
Zaidi soma hapa kwa kiingereza: http://www.dailymail.co.uk/news/article-1388834/Wife-daughter-disgraced-IMF-boss-arrive-court-appeal-bail-hearing.html#ixzz1MrCCmdJV

IKO WAPI HII??!

VIJISENTI VINAPOSHINDWA KUKUSAIDIA..

Mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF) bwana Dominique Strauss-Kahn ambaye pia ni mwanasheria,mwanasiasa na mwanauchumi wa kifaransa amewekwa jela Marekani kufuatia madai ya kutaka kumbaka mhudumu wa Hotel (Hotel Maid).Baada ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kufuatia kitendo hicho bwana Strauss-Kahn kupitia mwanasheria wake aliomba aachiwe kwa dhamana ya (vijisenti)  Dollar Million moja ($1m) mahakama ilikataa dhamana hio na kumrudisha rumande.


                                       Aliyekua mkurugenzi wa IMF-Dominique Strauss-kahn 

Kufuatia skendo hio mkuu huyo wa IMF amelazimika kujiuzulu wadhifa wake ambapo Umoja wa nchi za Ulaya (EU) wamesha tangaza kinyang'anyiro na wagombea wa awali ni kama ifuatavyo:-

  • Mohamed El-Erian, Egypt

  • Stanley Fischer, Israel

  • Gordon Brown, UK

  • Kemal Dervis, Turkey

  • Peer Steinbrueck, Germany

  • Montek Singh Ahluwalia, India

  • Christine Lagarde, France

  • Agustin Carstens, Mexico

  • Trevor Manuel, South Africa

  • Axel Weber, Germany
  • ETI JUMAMOSI TAREHE 21/05/2011 MWISHO WA DUNIA???!!

    Imeripotiwa kutokea wahubiri wa kidini jijini New York-Marekani kufuatia wanacho dai mwisho wa dunia ni tarehe 21/05/2011 ambayo ni siku ya Jumamosi.Wahubiri hao ambao wamekua wakifanya kazi hio bila kuchoka wametoa vielelezo mbali mbali kuthibitisha tukio hilo.Zaidi wamedai tukio hilo si lazima litokee wakati mmoja duniani kote kufuatia kutofautiana masaa lakini lazima iwe tarehe iliyo tajwa!!

    Ni matumaini yangu hayata tokea yale ya Kibwetere wa Uganda kuchoma moto waumini wake wanao sadikika  kufika 1000 ndani ya kanisa la '' Amri kumi za Mungu'' eti mwisho wa dunia umefika na kubaki yeye na bosi msaidizi wake  Bi Credonia Mwerinde nje mnamo Machi 17 mwaka 2000.Hata hivyo mpaka sasa haijulikani kama Kibwetere  na mwenzie wapo hai na polisi wa Uganda kwa kushirikiana na wale wa kimataifa (Interpol) bado wana mtafuta Kibwetere popote alipo Duniani. Pamoja na kua na maswali mia nane kidogo mie yangu macho!!

    Kwa habari zaidi soma hapa:http://uk.news.yahoo.com/preachers-prophesying-end-world-york-000338169.html

    Zaidi kuhusu Kibwetere soma hapa:http://www.culteducation.com/kibwetere.html