Nimeona si vibaya wasomaji wangu mkaipata hii habari japo imepita muda lakini HIV/AIDS bado tunayo katika jamii na mtu kama huyu ni mfano tu.Ni wazi kua japo ni siri kubwa lakini kuna watu wenye magonjwa kama huyu dada wanaojua ni wagonjwa (mabibi kwa mabwana) wanaambukiza wengine kwa maksudi.Baadhi yetu tunawajua ila tuna kaa kimya na kuona kama haituhusu, lakini ukweli ni kwamba inatuhusu sana maana ile ni 'chain' tu hata wewe unaweza pata UKIMWI kupitia mtu huyohuyo unaysema hakuhusu.Naomba nieleweke kua wale wanaowajua wathirika na wanasambaza virusi vya 'UKIMWI' kwa makusudi walipotiwe kwenye vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua za kisheria kwani si ustarabu.
Kusoma kisa kilichonifanya niandike haya bofya HAPA
Saturday, August 4, 2012
Monday, June 4, 2012
Latest News - Diesel Vs Petrol
Diesel engines used to be noisy, smelly and somewhat agricultural. Then car makers wised up, made the engines cleaner, more powerful and refined, and with diesel cheaper than petrol at the pumps, the fuel suddenly became more viable. Not for long. With the Chancellor making diesel pricier than petrol, choosing between the two fuel forms is now no longer as clear cut.
If it was purely down to miles per gallon, diesel would win. Easily. A Ford Fiesta 1.4 TDCi returns a quoted Combined consumption of 69mpg. The petrol equivalent of the same capacity does 49mpg.
But petrol hits back with the model’s purchase-price advantage. The petrol Fiesta in three-door Edge trim would set you back £12,195. The diesel version costs £12,995. And the difference isn’t going to get smaller. Ford Powertrain’s director Andrew Fraser explains: “Diesel engines are getting more expensive to build due to increased legislation. Last year a diesel particulate filter (DPF) had to be fitted, which required an injection upgrade. In 2015, they’ll have to abide by Euro VI emissions standards, so most diesel engines will need a Nitrogen Oxide trap. It’ll all add up to making the payback period for diesel longer.”
The addition of DPFs in particular has been contentious. Vanessa Guyll from the AA’s technical services says: “The DPF and exhaust gas recirculation mean diesels really aren’t viable for short journeys and town work. The DPF doesn’t get hot enough to clear itself out. We get called to about 700 breakdowns a month for blocked DPFs.
“For anyone who potters around town and doesn’t do journeys that are a minimum of 10 miles we wouldn’t advise a diesel. Any savings owners might make on road tax would be quickly wiped out by fixing problems with the emissions equipment if usage isn’t suitable.”
Wewe unasemaje?
Saturday, April 28, 2012
Thursday, April 19, 2012
MZEE WA VIJISENTI WA NIGERIA AFUNGWA MIAKA 13
Gavana wa zamani wa moja ya majimbo tajiri Nigeria, (Delta State) bwana James Ibori afungwa miaka 13 jela.Bwana Ibori alikamatwa mwaka 2010 Dubai kwa makosa ya kujipatia mamilioni kwa njia ya udanganyifu.Mheshimiwa huyo wa ugavana jimbo tajwa kwa miaka ya 1997-2007 baada ya kukamatwa alipelekwa nchini Uingereza ambako alikua ameweka baadhi ya pesa na kununua majumba ya kifahari kwa mahojiano zaidi na polisi mpaka kufikia uamuzi huo wa kufungwa miaka 13 baada ya kuthibitika.Sambamba na hilo mheshimiwa atafilisiwa kwa maslahi ya taifa hilo kubwa kabisa balani Afrika,hususani Afrika Magharibi.
Jeshi la polisi nchini Uingereza lilishangazwa na manunuzi ya gavana ambaye inasemekana mshahara wake ni 4000£= 10Million za Ki Tanzania kununua nyumba moja kwa gharama ya 2.2 million pounds sawa ma takribani Billion 2 na nusu za kitanzania, pia alinunua nyumba nyingine kwa £ 311,000 (UK), pia kanunua mansion South Africa kwa £3.2Million, Magari kadhaa aina ya Range Rovers kwa £600,000, Gari aina ya Bentley £120,000, Mercedes Maybach kwa Euro 407,000.
Kweli Africa raha huyu ni kiongozi mmoja tu!! Je serikali zetu zina pesa kiasi gani? (TAFAKARI......!!!!!)
Kwa habari zaidi soma HAPA
Jeshi la polisi nchini Uingereza lilishangazwa na manunuzi ya gavana ambaye inasemekana mshahara wake ni 4000£= 10Million za Ki Tanzania kununua nyumba moja kwa gharama ya 2.2 million pounds sawa ma takribani Billion 2 na nusu za kitanzania, pia alinunua nyumba nyingine kwa £ 311,000 (UK), pia kanunua mansion South Africa kwa £3.2Million, Magari kadhaa aina ya Range Rovers kwa £600,000, Gari aina ya Bentley £120,000, Mercedes Maybach kwa Euro 407,000.
Kweli Africa raha huyu ni kiongozi mmoja tu!! Je serikali zetu zina pesa kiasi gani? (TAFAKARI......!!!!!)
Kwa habari zaidi soma HAPA
Labels:
Gavana,
James Ibori,
Nigeria.,
Ubadhirifu wa mali ya uma
Tuesday, April 10, 2012
KUMBE POLISI NAO HUIBIWA!!!
Habari toka majuu (Kwa Malikia/UK aka Ukerewe) zinasema maelfu ya pauni za Uingereza aka Great Britain Pound (GBP) yaliyokua mikononi mwa polisi yaibiwa. Pesa hizo ni zile ambazo zilikamatwa kutokana na upatikanaji wake kuhusisha njia ya udanganyifu na kuhifadhiwa katika ghala yenye ulinzi mkali katika kituo kimoja cha polisi wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. Watu watatu walitiwa hatiani kuhusishwa na sakata hilo.Hata hivyo pesa hizo kiasi cha 113,000£ zapotea katika mazingira ya kutatanisha.Uchunguzi unaendelea na hakuna polisi wala raia aliyetiwa hatiani kutokana na upotevu huo..Inashangaza eti pesa ikaibiwa kituo cha polisi!!.Hivi polisi hazina bank accounts?.Kweli Duniani kuna mambo!!
Kwa habari zaidi soma HAPA
Kwa habari zaidi soma HAPA
Monday, April 9, 2012
MAZISHI YA KANUMBA KUFANYIKA LEO KINONDONI MAKABURINI BAADA YA MISA NA KUAGWA RASMI VIWANJA VYA LEADERS CLUB
RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
Msanii huyo ambaye atazikwa katika makaburi ya Kinondoni amefanyiwa utaratibu ambao utamwezesha kila mwenye kuhitaji kushiriki mazishi hayo kuweza kumuaga.
Mwili wa marehemu utachukuliwa kwa msafara kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili saa 2.30 asubuhi. Utapitishwa barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Kamati hiyo imetoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa mbili asubuhi kumuaga katika barabara ambazo atapitishwa . Saa 3.30 asubuhi mwili wa Kanumba utapokelewa viwanja vya Leaders ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal.
Saa 4.00 itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo inakadiriwa kuchukua dakika 60 na saa 5 itakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali. Saa 6.00 mchana ratriba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9.00 alasiri na baada ya hapo utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka makaburi ya Kinondoni.Msafara huo utapitia barabara ya Tunisia, utakatisha barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.
Sa 10.00 maziko yatafanyika kwa kufuata taratibu za imani ya marehemu. Kamati hiyo ya mazishi inayoongozwa na Gabriel Mtitu imewaomba wananchi watakohudhuria shughuli hiyo kwenda na maua ili kumuaga kwa heshima. Ibada na maziko vitafanyika kadri ya imani ya marehemu. Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.
K.N.Y GABRIEL MTITU MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI
Subscribe to:
Posts (Atom)



